Kwa mujibu wa maafisa wa congo wanasema kuwa idadi ya watu waliouawa kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyotokea kaskazini mashariki mwa congo huenda ikafika 200.
Maafisa wanasema kuwa idadi hiyo ni kutokana na idadi ya familia zilizofukiwa baada ya mfua kubwa kusababisha sehemu ya milima iliyokaribu kuporomoka.Idadi kubwa ya watu waliouawa ni wafugaji katika ziwa Albert.
Matumaini ya kuwapata manusura bado inakuwa ndogo kutokana na waokoaji kushindwa kuondoa mawe makubwa.
"Kuna watu wengine zaidi waliofukiwa ambao hatuna uwezo wa kuwaokoa"alisema naibu Gavana wa mkoa wa Ituri.
Sehemu nyingi za magharibi na kati mwa Afrika zinakumbwa na maporomoko ya Ardhi kutokana na miti mingi kukwatwa na jamii zinazoishi katika maeneo hayo.
Janga hili limetokea baada ya janga lingine kutokea hivi karibuni nchini Sierra Leone ambapo watu zaidi ya 400 kuuawa na wengine 600 kutojulikana mahali walipo.
0 Maoni