TANGAZA HAPA

KOREA KASKAZINI:Siku chache zijazo tunampango wa kushambulia kisiwa cha marekani cha Guam

marekani


Huku majibizano ya vita yakiendelea kati ya korea na marekani korea wamesema kuwa mpango wao wa kutupa makombora katika kisiwa cha marekani cha Guam utakuwa tayari hivi karibuni.

Mpango huo ukiidhinishwa na Kim Jong-un korea inasema itapitisha makombora ya Hwasong-12 katika anga yake na kuanguka baharini kilometa 30 kutoka katika kisiwa cha Guam.

Marekani wameionya Korea ya Kaskazini ikisema vitendo vyake vinamaanisha kuwa ndo itakuwa mwisho wa utawala wa nchi hiyo.

Korea ilipuuzia onyo la Rais Donald Trump kuwa itashambuliwa vikali.

"Korea kaskazini itashindwa vibaya endapo itaingia vitani na marekani pamoja na washirika wake"Alisema waziri wa ulizi wa marekani Jim Mattis.

Korea kaskazini ilisema siku ya jumatano kuwa inafanya mpango wa mashambulizi katika kisiwa cha marekani cha Guam kilina na kambi ya Jeshi la anga la marekani pamoja na wanajeshi takribani 163,000.



Jiunge na mauricemackytz.com sasa

Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni