TANGAZA HAPA

Marekani na Korea Kusini kuungana kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja

usa
Marekani na korea kusini zimeungana kufanya mazoezi ya kijeshi ambayo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kujiweka sawa na mashambulizi yoyote yanayoweza kujitokeza.

Korea kaskazini ytayari imeshalaani kitendo hicho na kusema kuwa ni kama kumwaga mafuta kwenye moto.Wiki iliyopota Korea Kaskazini ilionyesha kulegeza kamba baada kutishia kuwa itarusha makombora kwenye kisiwa cha marekani cha Guam lakini baadae ikasema kuw itafuatilia mienendo ya marekani.

korea


Marekani imesema kuwa mazoeazi itahusisha wanajeshi 17,500 wa Marekani na yatadumu kwa muda siku kumi.Korea Kusini hutuma wanajeshi 50,000 huku marekani ikituma kati ya wanajeshi 25,000 na 30,000.Mazoezi hayo hufanyika mara mbili kwa mwaka yanayoshirikisha idadi kubwa ya wanajeshi na zana za vita.

Mazoezi hayo hujumuisha Ardhini,baharini pamoja na angani,mazoezi hayo ambayo hufanyika Korea Kusini pia hujumuisha jinsinya kukabiliana na mashambulizi ya kemikali.na pia mazoezi hayo hushirikisha wanajeshi kutoka nchi washirika ambapo mwaka uliopita nchi nyingine tisa ziliungana nao.

usa



Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni