TANGAZA HAPA

Meli ya kivita ya Marekani yagongana na meli ya mafuta Singapore

uss john maccain
Jeshi la majini nchini marekani limesema kuwa wanajeshi 10 hawajulikani walipo na wengine watano wamejeruhiwa baada ya meli ya kivita ya marekani kugongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore.


Meli ya kivita ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati ilipogongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.bado shughuli za kuwatafuta waliopotea zinaendele.

Ripoti zinasema kuwa meli hiyo ilikumbwa na uharibifu .Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore,walinzi wa pwani pamoja na jeshi la Malaysia wanaendelea na shughuli za uokoaji.

Meli hiyo ya mafuta iliripotiwa kuwa na uzito mara tatu wa uzito wa meli ya kivita ya USS John MacCain.pia taarifa zinasema ilikuwa haijabeba mafuta kwa wakati huo.

Mwezi juni mabaharia saba wa marekani waliuawa wakati wa meli ya kivita ya USS Fitzgerald ilipogongana na meli ya  mizigo kwenye bahari ya Japani karibu na bandari ya Yokosuka.


Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni