Mkuu wa mikakati wa Rais Donald Trump katika ikulu ya White House Steve Bannon Amefuta kazi.
Katibu wa mawasiliano na wanahabari katika ikulu hiyo Sarah Huckabee Sanders amethibitisha kuwa ijumaa ilikuwa siku ya wisho ya bw.Bannon kazini.Alikuwa wa tovuti ya Breitbart.com na alisaidia pakubwa kueneza ujumbe wa "American First" (Marekani Kwanza) wakati wa kampeni za urais zilizofanyika mwaka jana.
Bw Bannon anadaiwa kushindania udhibiti wa ikulu thidi ya mirengo ya watumishi wenye misimamo ya wastani ikulu wakiwemo baadhi ya jamaa wa trump.
Bw Trump alianzisha uvumi juu ya Bannon lipoulizwa kuhusu mustakabali wake wiki iliyopita lakini akajibu "Tutasubiri Tuone"
Bannon alinukuliwa akipuuzilia mbali wazo la kutumia wanajeshi kutatua mzozo dhidi ya korea kaskazini jambo lililotazamwa kama kwenda kinyume na msimamo wa Trump.
Bannon aliambia jarida la American Prospect kuwa marekani ilikuwa katika vita vya kiuchumi na China kwamba analenga kuondoa watu wenye msimamo wa wasatni serikali ya Trump ambao anaamini wanamsimamo usio mkali dhidi ya China.
Lakini baadae bw Bannon alisema kuwa aliwaambia washirika wake kwamba alidhani alikuwa akiongea akipiga gumzo tu ila hakudhani kuwa atanukuliwa.
Jiunge na mauricemackytz.com sasa
0 Maoni