Rais wa Zambia Edga Lungu
Rais wa Zambia Edga Lungu amesema ni lazima wananchi wake wapime virusi vya ukimwi na kujua ni jinsi gani wanaweza kufanya ili kutokuambukiza wengine.
Rais huyo ametoa uamuzi huo baada ya nchi yake kuwa ni moja wapo ya nchi yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kusini mwa bara la Africa ikiwa na asilimia 11.6 huku watu wenye umri kati ya miaka 15 na 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.
Rais Lungu amesema kupima ukimwi na kupewa ushauri na matibabu siyo jambo la hiari bali ni lazima kwakuwa kufanya hivyo ianweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Jiunge na mauricemackytz.com sasa
0 Maoni