Kombora aina ya S-200 Angara |
kombora la kutungua ndege lililoibiwa nchini urusi limelipuka na kuwaua watu wawili na kujeruhi mmoja.
Kombora hilo lenye urefu wa mita 10 (futi 35) lililoundwa wakati wa enzi za usovieti lililipuka kwenye kiwanda cha kutengeneza bidhaa mpya kutoka kwenye bidhaa kuukuu mashariki mwa urusi.
Vyombo vya habari nchini Urusi vinafahamisha kuhusu mlipuko wa kombora hilo kubwa katika mji wa chita baada ya video ya ,lipiko huo iliyokuwa imepigwa na mtu mmoja kupitia kamera yake ya gari kuipakia kwenye Youtube.
Makombora hayo yamekuwa yakitumika katika miaka ya 1960 lakini siku hizi nafasi yake imeanza kuchukuliwa na makombora aina ya S-300 na S-400.
Tovuti ya by24.org linasema kuwa kombora hilo liliibiwa kwenye kambi ya jeshi na watu wasiojulikana na kuuziwa mkuu wa kiwnda hicho.
Lililipuka wakati wakiwa wanajaribu kulibomoa na haijajulikana lilifika vipi katika kiwanda hicho.
Tovuti ya The Insider inasema kuwa wafanyakazi wa dharura walipata kombora lingine aina S-200 ambalo lilikuwa halijabomolewa.
Kisa hicho kimezua mijadala mikali katika mitandao ya kijamii wengi wakishangaa ilikuwaje mpka kombora hilo likafika katika kiwanda hicho.
"Tuna silaha nyingi hivi kuukuu nchini urusi kiasi kwamba watu wanaziuza kama vyuma vikukuu"Aliandika mmoja wa watu kwenye mtandao wa VKontakte alisema hilo linaweza kusababisha madhara makubwa.
Jiunge na mauricemackytz.com sasa
0 Maoni