TANGAZA HAPA

Rais Magufuli ameteua makatibu wapya wa wizara

Rais Magufuli amemteua aliekuwa inspekta Jenerali wa Polisi (IGP-Mstaafu) Ernest Mangu kuwa Balozi.

Bw mangu pamoja na aliekuwa katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje na ushirikino wa Afrika Mashariki ambaye amefanywa kuwa balozi Dkt. Aziz Mlima watapangiwa vituo vya kazi baada ya utaratibu kukamilika.

Rais Magufuli amefanya uteuzi huo wakati alipokuwa akifanyia mabadiliko makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika serikali yake.

Rais magufuli amefanaya mabadiliko hayo baada ya kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri.

Pia rais Magufuli ameteua wakuu wapya wa mikoa.

Orodha ya Makatibu wakuu na Naibu katibu wakuu ni kama ifwatavyo:-

  1. 1.    Ofisi ya Rais Ikulu.
  • Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata

  1. 2.    Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  • Katibu Mkuu (Utumishi)     – Laurian Ndumbaro
  • Naibu Katibu Mkuu            - Dorothy Mwaluko

  1. 3.    Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  • Katibu Mkuu                        - Mhandisi Mussa Iyombe
  • Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
  • Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda

  1. 4.    Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
  • Katibu Mkuu                        - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
  • Naibu Katibu Mkuu            - Bi. Butamo Kasuka Phillipo

  1. 5.    Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
  • Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
  • Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
  • Katibu Mkuu(Sera na Uratibu)      - Prof. Faustine Kamuzora

  1. 6.    Wizara ya Kilimo.
  • Katibu Mkuu                        - Mhandisi Methew Mtigumwe
  • Naibu Katibu Mkuu            - Dkt. Thomas Didimu Kashililah

  1. 7.    Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
  • Katibu Mkuu (Mifugo)        - Dkt. Maria Mashingo
  • Katibu Mkuu (Uvuvi)           - Dkt. Yohana Budeba

  1. 8.    Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
  • Katibu Mkuu (Ujenzi)         - Mhandisi Joseph Nyamuhanga
  • Katibu Mkuu (Uchukuzi)    - Dkt. Leonard Chamriho
  • Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo
  • Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete

  1. 9.    Wizara ya Fedha na Mipango.
  • Katibu Mkuu                                    - Doto James Mgosha
  • Naibu Katibu Mkuu (Utawala)       - Bi. Susana Mkapa
  • Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban
  • Naibu Katibu Mkuu (Sera) - Dkt. Khatibu Kazungu

10.Wizara ya Nishati.
  • Katibu Mkuu                        - Dkt. Hamis Mwinyimvua

11.Wizara ya Madini.
  • Katibu Mkuu                        - Prof. Simon S. Msanjila
           
  1. 12.   Wizara ya Katiba na Sheria.
  • Katibu Mkuu                        - Prof. Sifuni Mchome
  • Naibu Katibu Mkuu            - Amon Mpanju

  1. 13.   Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  • Katibu Mkuu              - Prof. Adolf F. Mkenda
  • Naibu Katibu Mkuu   - Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi

14.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
  • Katibu Mkuu                        - Dkt. Florence Turuka
  • Naibu Katibu Mkuu            - Bi. Immaculate Peter Ngwale

  1. 15.   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  • Katibu Mkuu                        - Meja Jen. Projest A. Rwegasira
  • Naibu Katibu Mkuu            - Balozi Hassan Simba Yahaya

16.Wizara ya Maliasili na Utalii.
  • Katibu Mkuu                        - Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
  • Naibu Katibu Mkuu            - Dkt. Aloyce K. Nzuki

17.Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
  • Katibu Mkuu                        - Dorothy Mwanyika
  • Naibu Katibu Mkuu            - Dkt. Moses M. Kusiluka

18.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
  • Katibu Mkuu                                    - Prof. Elisante Ole Gabriel
  • Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye
  • Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija

  1. 19.   Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
  • Katibu Mkuu                                    - Dkt. Leonard Akwilapo
  • Naibu Katibu Mkuu            - Prof. James Epiphan Mdoe
  • Naibu Katibu Mkuu            - Dkt. Ave-Maria Semakafu

  1. 20.   Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
  • Katibu Mkuu (Afya)             - Dkt. Mpoki Ulisubisya
  • Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)    - Bi. Sihaba Nkinga.

  1. 21.   Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  • Katibu Mkuu                                    - Bi. Suzan Paul Mlawi
  • Naibu Katibu Mkuu            - Nicholaus B. William

  1. 22.   Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
  • Katibu Mkuu                        - Prof. Kitila Mkumbo
  • Naibu Katibu Mkuu            - Mhandisi Emmanuel Kalobelo

Wakuu wapya wa Mikoa:-

Bw Alexander Pastory Mnyeti kuwa mkuu wa mkoa wa manyara nafasi iliyoachwa na Bw Joel Bendera ambae amestaafu.

Bw Joackim Leonard Wangabo kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa nafasi iliyoacha na kamishna wa polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.

Bw Robert Gabriel Luhumbi kuwa mkuu wa mkoa wa Geita nafasi iliyoachwa na meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.

Bw Adam Kigoma Malima kuwa mkuu wa mkoa wa Mara nafasi iliyoachwa na Dkt. Charles Mlingwa.

Bi Christine Solomon Mndeme kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma nafasi iliyoachwa na Bw Jordan Rugimbana.

Bw Gelasius Gasper Byakanwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mtwara nafasi iliyoachwa na Bi Halima Dendego.


Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni