TANGAZA HAPA

Mtuhumiwa wa kosa la mauaji ajilipua mahakamani wakati kesi yake ikisikilizwa {Video+}

Mtuhumiwa ma kosa la mauaji ajilipua mahakamani wakati kesi yake ikiwa inaendelea kusikilzwa nchini Ukraine.

Mtuhumiwa huyo amejilipua yeye pamoja na mtuhimiwa mwenzie wakati wa kesi inayowakabili ya kuua kwa kukusudia mjini Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa polisi imesemekana kuwa watu wawili wameuawa na wengine tisa wamejeruhiwa katika tukio hilo wakiwemo washtakiwa wawili,walinzi wawili,mawakili watatu wa serikali,pamoja naraia wawili waliokuwa wakisikilza kesi hiyo.


Mtuhumiwa huyo na wenzake watatu wanatuhumiwa kulifyatulia risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016.
Kwa mujibu wa mtandao wa Ukrainska Pravda taarifa zinasema mtuhumiwa mmoja alitoa maguruneti mawili wakati kesi ikiendelea mahakamani hapo na kuyalipua.
Gazeti hilo likimnukuu Msemaji wa Jeshi la Polisi mjini Nikopol, Yaroslav Trakalo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alichukua hatua hiyo baada ya kusikia kwamba kesi hiyo inaahirishwa na kwamba watuhumiwa wanarudishwa rumande.



Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni