TANGAZA HAPA

Trump amshutumu waziri mkuu wa Uingereza

Rais wa Marekani Donald Trump amemwambia waziri mkuu wa Uingereza Theresa May kuangazia ugaidi nchini Uingereza badala ya kumkosoa kwa kusambaza video za kundi la mrengo wa kulia la uingereza ambalo linaeneza chuki.

Bw Trump alisema haya kupitia mtandao wake wa Twitter "Usiniangazie sana mimi,angazia ugaidi unatekelezwa na makundi yenye itikadi kali ambao unatekelezwa nchini humo"
Awali rais Trump alitum video tatu zenye chuki mbazo zilisambazwa ambazo zilisambazwa kwenye mtandao wa Twitter na makundi hayo kutoka nchini Uingereza.Ambapo msemaji wa Bi May alisema kuwa ni makosa Rais Trump kufanya hivyo.

Kanda za video ambazo likuwa zimetumwa na rais trump zilikuwa zimechapishwa na Jayda Fransen naibu kiongozi wa kundi la Uingereza la Britain First kundi lililoanzishwa na mwnachama wa zamani wa kundi la mrengo wa kulia wa chama cha Uingereza cha BNP.

Wanasiasa nchini Uingereza wamekosoa ujumbe huo wa bw Trump akiwemo askofu mkuu wa Cantebury Justin Welby ambaye alisema inakera kwamba rais Trump aliamua kulipatia sauti kundi lenye itikadi kali la mrengo wa kulia.

Hatua hiyo imezua hisia kali huku baadhi ya wananchi wakitka ziara ya Rais Trump nchini Uingereza kufutiliwa mbali japokuwa ofisi ya waziri mkuu inasema kuwa kuwa zira hiyo bado itafanyika.


Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram 

Chapisha Maoni

0 Maoni