TANGAZA HAPA

AFRIKA KUSINI: Kanisa moja laruhusu waumini kunywa pombe wakati wa ibada

Kupitia NCA TV ya Afrika Kusini imeonyeshwa taarifa ya kanisa jipya lililopo nje kidogo ya mji wa Johannesburg ambapo imeonyesha waumini pamoja na askofu wakinywa pombe wakati ibada ikiwa inaendelea.

Askofu mkuu wa kanisa hilo lijulikalo kama Kabhula askofu Itiehth Makiti amesema lengo kuu la kanisa hilo ni kupokea watu ambao wametengwa na kukataliwa na jamii zao kutokana na tabia zo za kunywa pombe.

Amesema kuwa yeye kama kiongozi wa kanisa hilo analiongoza kwa kuonyesha mfano hivyo hata yeye kabla ya kuongoza ibada anakunywa kilevi anachokipenda ambapo waumini wapya hukaribishwa na maombi na kunywesha aina ya pombe wanayoitaka.


Jiunge na mauricemackytz.com sasa
Unaweza kutufuatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii Facebook Twitter pamoja na Instagram

Chapisha Maoni

0 Maoni