Sehemu ya Helikopta ya kijeshi ya Marekani imeanguka katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko kwa watu wa eneo hilo.
Sehemu hiyo ya mlango ilianguka katika uwanja wa shule moja ambapo imesababisha majeraha madogo kwa mwanafunzi mmoja.
Kisiwa cha Okinawa ni kambi kubwa zaidi ya jeshi la Marekani nchini Japan.
Katika miaka ya hivi karibuni ajali kadhaa na visa vya uhalifu vimesababisha kuwepo upinzani dhidi ya kambi hiyo ya Marekani.
Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa dirisha moja ya Helikopta zake ilianguka kwenye uwanja wa michezo iliyopo nje ya kambi yake ya jeshi la wanaanga.
Jiunge na mauricemackytz.com sasa
0 Maoni