Yamkini watu 20 wanahofiwa kuuawa baada ya hoteli maarufu ya Intercontinental iliyoko Kabul nchini Afghanistan kuvamiwa na magaidi.
Wanajeshi nchini humo wamekuwa wakipigana gorofa baad ya gorofa ili kuchukua udhibiti wa hoteli hiyo ya kifahari mjini Kabul baada ya kuvamiwa na wapiganaji waliokuwa na silaha nzito.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo amesema kuwa magaidi wawili (2) kati ya wanne (4) waliovamia hoteli hiyo tayari wameshauawa.
Washambuliaji hao walivamia hoteli hiyo na kuanza kuwamiminia risasi wageni na wafanyakazi pamoja na kurusha magruneti.
Taarifa nyingine zinasema kuwa wakati uvamizi huo ukiwa unaendelea hoteli hiyo ilikuwa ikiandaa kongamano la Teknolojia ya mawasilino (IT) iliyokuwa ikihudhuriwa na maafisa wa mikoa.
Shambulio hilo limetokea siku kadhaa baada ya ubalozi wa Marekani mjini Kabul kutoa taadhari ya uwezekano wa kutokea shambulio la kigaidi litakalolenga mahoteli kadhaa mjini hapo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini humo Nasrat Rahimi ameiambia BBC kuwa walinda usalama wamechuku udhibiti wa gorofa ya kwanza ya hoteli hiyo.
0 Maoni