Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-Un, ametangaza kusitishwa kwa mda shughuli zake za kufanya majaribio ya silaha zake za Kinyuklia.
Kim Jong-Un amedai kwamba hamna haja ya kufanya tena majaribio kwa sababu nchi yake tayari imefanikiwa katika malengo yao ya kuwa wamiliki wa zana za kinyuklia
Tangazo hilo linajiria wakati kuna harakati za kuharibu kufanikisha maandalizi ya mikutano inayotarajiwa kufanyika baina ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na raia wa Marekani Donald Trump.
Msururu wa majaribio ya makombora ya kinyuklia yaliyofanywa na Korea kazkazini mwaka jana yalizua taharuki miongoni mwa majirani zake hasa Japan na Korea Kusini na vile vile mshirika wao mkuu Marekani.
Pamoja na malumbano ya maneno makali baina yao, Marekani imekuwa mstari wa mbele kuhimiza vikwazo chungu nzima vya kiuchumi huku nchi zinazokiuka vikwazo hivyo nazo zikifuatiliwa kwa karibu sana.
Maandalizi ya mkutano kati ya trump na Kim Jon Un yalifannikiswa na mkurugenzi wa shirika la ujasusi Marekani CIA ,Mike Pompeo ambaye aliunda "uhusiano mzuri" na kiongozi huyo wa Korea kaskazini walipokutana wiki iliyopita, kwa niaba ya Rais Trump katika ujumbe wake wa Twitter.
Akithibitisha taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari kuhusu mkutano huo wa siri mjini Pyongyang, Trump amesema mkutano ulimalizika "bila ya tashwishi".
Ziara hiyo ya kushtukiza inadhihirisha mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Korea kaskazini tangu 2000.
Rais Donald Trump anatarajiwa kuandaa mkutano na Bwana Kim kufikia mwezi Juni. Bado ratiba inaandaliwa, rais wa Marekani amesema.
Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwengine kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka.
Bwana Trump alikuwa amekiri kufanyika kwa mazungumzo ya hadhi ya juu na Pyongayng.
''Tumekuwa na mazungumzo ya moja kwa moja , katika ngazi za juu'', Bwana Trump alisema mjini Florida ambapo alikuwa anakutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Rais huyo aliongezea kuwa aliunga mkono mazungumzo kati ya Korea kusini na kaskazini kuzungumzia makubaliano ya amani ya kumaliza vita vya Korea vya 1950-1953
Korea Kusini imetoa ishara kwamba itaangazia suluhu rasmi ya kumaliza mgogoro huo. Rais wa Korea Kusini Moon Jae in na bwana Kim wanatarajiwa kukutana mwisho wa mwezi Aprili.
0 Maoni