Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini mswada wa Sheria ya Uhalifu wa Kompyuta na Mtandaoni ya mwaka 2018 kuwa Sheria, hatua hii itatoa adhabu kali kwa watakaopatikana na makossa ya mtandaoni.
Sheria hiyo inatoa adhabu ya faini dola 50,000 za Marekani {Sawa na zaidi ya Tsh milioni 100} au kifungo cha miaka miwili jela, au adhabu zote mbili, kwa atakayepatikana na kosa la uenezaji wa habari za uzushi.
Mtu atakayepatikana na kosa la kueneza taarifa ambazo zinaweza kuzua taharuki au kuzua vurugu atafungwa jela zaidi ya miaka kumi.
0 Maoni