TANGAZA HAPA

KOREA KASKAZINI hatiani kuvunja mkutano wake na MAREKANI


Serikali ya Korea Kaskazini imesema huenda ikaufutilia mbali mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini (KCNA) limemnukuu Naibu Waziri wa mambo ya nje, Kim Kye-gwan akisema kuwa “sharti hilo litawabana wao hivyo hawatakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itawalazimu kutafakari upya iwapo watakubali mkutano huo.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Jumanne ya Juni 12, 2018.

Chapisha Maoni

0 Maoni