Afisa upepelezi wilaya ya Mkinga mkoani Tanga anashikiliwa na polisi kwa kudaiwa kuwaachia huru watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokamatwa na mali za magendo zenye thamani zaidi ya shilingi Bilioni 1.2.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari mgumba amesema septemba 09, 2022 walikamata jahazi lililobeba baro 170 za vitenge zilizokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 570 na watu wanane waliohusika na usafirishaji huo huku septemba 11 kamati ya ulinzi walikamata watu 20 na malori mawili aina ya fuso yakiwa na baro 90 za vitenge kila moja.
"Nimeshangazwa kuona watuhumiwa wote wanne waliokamatwa na jahazi wameachiwa huru bila taarifa na hawajafunguliwa kesi kama vile hakuna walichofanya huku watuhumiwa 15 kati ya 20 ambao walikamatwa 170 za vitenge nao wameachiwa huru ingawa wamefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi" Alisema Omari Mgumba.
Mgumba anasema alipofanya kikao na kamati hiyo ndipo alipobaini afisa upelelezi wilaya ya Mkinga ndie aliehusika kuwaachia watuhumiwa hao ambae anasema alipewa maelekezo na afisa upelelezi mkoa ambae hakuwa kwenye kikao hicho.
Aidha mkuu wa mkoa amesema afisa upelelezi huyo tayari yupo ndani na sheria itafata mkondo wake.
0 Maoni