TANGAZA HAPA

Ajinyonga kisa madeni ya VICOBA

           mtzonline255.tk

Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Enea Mkimbo miaka (55) mkazi wa Kihela Kilolo manispaa ya Iringa amejinyonga leo Septemba 14, 2022 chanzo kikiwa ni kuzidiwa na madeni ya VICOBA na usumbufu kutoka kwa wanakikundi wenzie.

Mwenyekiti wa mtaa huo Michael Mlalwe amesema kuwa marehemu Enea ambae ameacha mume na watoto watano jana Septemba 13, 2022 alifatwa na wanakikundi wenzie wakimshinikiza kutoa pesa ambapo baada ya tukio hilo Enea aliaga anaenda kulala kwa mama yake mzazi eneo la Ilembila na badala yake aliingia jikoni na kujinyonga kwa kutumia kanga.

Chapisha Maoni

0 Maoni