TANGAZA HAPA

Akamatwa akisafirsha madawa ya kulevya kwa gari la mafuta

                              

Jeshi la polisi mkoa nia Arusha limewakamata watu 38 wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ambapo mmoja kati yao amekuta akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kwa kutumia lori la mafuta.

Akitoa taarifa hiyo leo Septemba 11, 2022 kamanda wa polisi mkoani Arusha kamishna msaidizi wa polisi ACP Justine Masejo alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti kwenye uperesheni iliyofanyika kuanzia Septemba 5 hadi septemba 10, 2022 iliyoendeshwa na mkuu wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha.

Kamanda Masejo amesema kuwa tarehe 10.09.2022 muda wa saa 12:30 aubuhi huko katika mta wa Kikwe uliopo katika wilaya ya Kikwe wilaya ya Arumeru jeshi hilo la polisi lilimkamata mtu mmoja aitwa Allen Wilbard Kasamu (49) dereva mkazi wa Sue jijini Arusha akiwa anasafirisha madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni mirungi yenye uzito zaidi ya kilo 390.75.

Chapisha Maoni

0 Maoni