Chama cha soka Argentina (AFA) kimeahirisha mechi zote za soka ambazo zilikuwa zichezwe leo ijumaa Septemba 2, 2022 kutokana na kufeli kwa jaribio la mauaji la makamu wa raisi wa taifa hilo Cristina Fernandez de Kirchner (69).
Maamuzi hayo yamekuja baada ya kuonekana shambulio hilo ni tishio kwa usalama wa nchi ambalo limetokea wakati Makamu huyo wa raisi akirejea nyumbani kwake akitokea mahakamani Buenos Aries ambapo alikana mashataka ya rushwa yanayomkabili.
Tukio hilo limetokea alhamisi baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 35 kutoa bastola na kutaka kufyatua risasi lakini bastola hiyo iliyokuwa na risasi tano iligoma kufyatua rasasi na kujikuta kuishia mikononi mwa polisi.
Bi Cristina Fernandez de Kirchner ni makamu wa raisi wa 37 ambapo ameshikilia nafasi hiyo toka mwaka 2019 na amewahi kuwa raisi wa Argentina wa 54 toka mwaka 2007 - 2015 na alikuwa mke wa raisi wa Argentina Néstor Kirchner aliedumu madarakani 2003 - 2007 kisha mkewe kuchukua nchi.
0 Maoni