Mamlaka ya udhibiti na usafirishaji ardhini (LATRA) imesema kampuni za usafirishaji kwa njia ya mtandao Bolt na Uber zinatarajia kurejea kutoa huduma za usafirishaji nchini.
Yamesemwa hayo leo jumatatu Septemba 12, 2022 na mkurugenzi mkuu LATRA Habibu Suluo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
LATRA imetoa taarifa hiyo wakati kampuni hizo kwa nyakati mbili tofauti walisitisha kutoa huduma na za magari na kuacha bodaboda na pikipiki pekee.
Suluo amesema wamesikia kilio cha kampuni hizo na wameitana na kukaa meza moja kwa mazungumzo na tayari yametatua tatizo ili kurejesha huduma.
"Tuliwaita wakaja na wawakilishi wao wa Afrika kukaanza Septemba 5-8, 2022 tumemaliza mazungumzo ambapo kuna taarifa tutanataka watuletee kiandishi ili kutoa maamuzi na leo ndio siku ya mwisho tuliokubaliana na tutatoa maamuzi wote ikiwemo umoja wa madereva teksi (TODA)" Alisema Suluo.
0 Maoni