TANGAZA HAPA

CANADA : 10 wauawa, 15 wajeruhiwa kwa kuchomwa kisu


Polisi nchini Canada inawasaka washukiwa wawili katika tukio ambalo watu (10) waliuawa na wengine (15) wakijeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika eneo moja la jamii la kiasili lisilo na wakazi wengi.

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema mauaji hayo katika eneo la Saskatchewan ni yakutisha na kuvunja moyo.

Polisi inawataja washukiwa wawili Damien Sanderson (31) na Myles Sanderson (30) na kutoa picha zao pamoja na maelezo lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu nia yao wala kuhusu wahanga.

Polisi walisema baadhi ya wahanga inaonekana kuwa walilengwa na wengine walishambuliwa bila mpangilio.

Mauaji hayo ya watu wengi ndio makubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya karibuni nchini Canada.

Chapisha Maoni

0 Maoni