Polisi nchini Canada wamesema kuwa mmoja kati ya washukiwa wawili wa mauaji ya kutumia kisu yaliyotokea jumapili huko Saskatchewan amepatikana akiwa amefariki.
Mwili wa Damien Sanderson (31) ulipatikana katika eneo la James Smith Cree Nation nyumbani kwa athirika kadhaa walisema
Washukiwa hao wawili walikuwa ndugu na polisi wanasema Myles Sanderson bado anaaminika kujificha katika jiji la Regina.
Siku ya jumapili watu 10 waliuawa kwa kuchomwa visu na wengine 18 kujeruhiwa katika moja ya matukio mabaya zaidi ya unyanyasaji katika historia ya hivi karibuni ya nchi ya Canada.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la mashambani la Saskatchewan katika mji wa Regina ambao ndi mji mkuu wa jimbo hilo ambapo washukiwa walionekana mara ya mwisho .
Maafisa wa polisi katika mikoa mitatu Saskatchewan,Monitoba na Alberta wanahusika katika msako huo.
0 Maoni