TANGAZA HAPA

Cardi B ahukumiwa siku 15 kuhudumia jamii

Staa wa muziki Cardi B amekiri makosa mawili yanayotokana na ugomvi katika klabu za utupu kama makubaliano ambayo yanamaanisha kuwa ataepuka kesi ya kufungwa jela.

Rapa huyo alikiri kosa la shambulio la kiwango cha tatu na kusababisha hatari kwa kiwango daraja la pili na alihukumiwa kifungo cha siku 15 katika huduma ya jamii,huku mashtaka mengine 10 yakitupiliwa mbali.

"Nimefanya maamuzi mabaya katika siku zangu zilizopita ambayo siogopi kukabiliana nayo na kuyasimamia"Alisema Cardi B

Mahakamani kijana huyo mwenye umri wa miaka (29) alikiri kuandaa na kushiriki katika mashambulizi mawili dhidi ya wafanyakazi wa klabu ya usiku ya Angels huko New York mnamo 2018.

Kulingana na mamlaka matukio hayo yalikuwa na ugomvi kati ya Almanza na wadada wawili mmoja wao aliamini kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe rapa Offset.




Chapisha Maoni

0 Maoni