Klabu ya nchini Uingereza Chelsea imefikia makubaliano ya kuachana na meneja wa kikosi chao Thomas Tuchel baada ya kuwa na mwenendo usioridhisha.
Tuchel aliteuliwa Januari 26,2021 kuchukua nafasi ya Frank Lampard na kuiongoza klabu hiyo kutwaa taji lao la pili la ligi ya mabingwa barani ulaya,UEFA super cup na Fifa Club world cup.
Klablu ya Chelsea ilitoa taarifa yake na kusema "Kwa niaba ya kila mtu katikla klabu ya Chelsea FC,klabu ingependa kuwekia rekodi ya shukrani zake Thomas na wafanyakazi wake kwa juhudi zao zote wakati wakiwa na Klabu.Thomas atakuwa na nafasi katika historia ya Chelsea baada ya kushinda Ligi ya mabigwa , kombe la super cup na kombe la dunia la klabu wakati wake hapa."
0 Maoni