TANGAZA HAPA

DODOMA: Akamatwa kwa kutupa mtoto mchanga

         mtzonline255.tk

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linamshikilia binti mmoja aliefahamika kwa jina la Nasra Khalifa (24) mkazi wa chamwino ambae anadaiwa kwa kutupa mtoto mchanga aliejifungua ambae aliokotwa akiwa amefariki baada ya wananchi kutoa taarifa juu ya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Dodoma ACP Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea leo Septemba 14, 2022 katika eneo la uhindini lililopo katikati ya jiji la Dodoma na kusema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alisema amefanya tukio hilo baada ya mwenye ujauzito kumkataa.

"Mtuhumiwa tuliemkama sasa hivi anaitwa Nasra Khalifa alienda kupata matibabu ya kiafya katika kituo cha makole na kidai alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo na kwamba alikuwa akiharisha na kutapika na wakati akiwa anapatiwa matibabu aliomba kwenda msalani,"

"Mtuhumiwa huyo alifungiwa mlango na alitumia muda mrefu kitu ambacho kiliwapa wauguzi mashaka na walipokuwa akimuomba afungue mlango alikuwa akikaidi na mda mfupi baadae alijifungu mtoto wa kiume"Alisema kamanda wa polisi

Aidhaa aliongeza kwa kusema baada ya kujifungua mtoto huyo alijitahidi kumtumbukiza kwenye tundu la choo mtoto huyo na hakufanikiwa baada ya kuokolewa na mtoto huyo alikuwa tayari amekisha fariki dunia huku mtuhumiwa akidai kuwa amefanya hivyo baada ya mtu aliempa ujauzito kutokuwa na maelewano nae mazuri.


Chapisha Maoni

0 Maoni