Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafuzi wa chuo cha St. John Winfrida Michael (24) baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julias Gervas (26) ambae ni mwanafunzi wa chuo hichohicho.
Kamanda Otieno amesema kuwa sababu ikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi baada ya Julias kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora.
"Hilo tukio limejitokeza ni wivu wa kimapenzi kijana kumchoma kisu mpenzi wake baadae alitaka kujichoma kisu lakini akawa amejijeruhi tu na kwasasa anaendelea na matibau katika hospitali ya rufaa ya Dodoma"Alisema kamanda Otieno
0 Maoni