Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Athanas Rugambwa (62) mkazi wa Muganza wilayani chato mkoani Geita kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa miaka nane (8) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Katema.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo hii Septemba 15, 2022 kamanda wa polisi mkoani Geita Henry Mwaibambe alisema mtuhumiwa huyo ni katekiska na alikuwa akimfundisha mtoto huyo masomo ya dini.
Alisema mtuhumiwa huyo alimvizia mtoto huyo akiwa kwenye mafundisho ya dini kanisani na kumuita ofisini kwake kisha kumbaka.
0 Maoni