TANGAZA HAPA

KENYA : Mahakama ya juu kutoa uamuzi leo

 


Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajia kutoa uamuzi wake juu ya pingamizi la matokeo ya uraisi uliofanyika mwezi uliopita.

Naibu raisi William Ruto alitangazwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa na idadi ya kura milioni 7.1 huku mpinzi mwenzake na mwanasiasa mkongwe Raila Odinga alipata kura milioni 6.9 na kupinga matokeo hayo.

Raila Odinga aliwasilisha maombi ya kukataa matokeo katika mahakama ya juu ya Kenya akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika mchakato wa kujumlisha kura na kudai kuwa alikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa alishinda uchaguzi wa Agosti 9,2022.


Chapisha Maoni

0 Maoni