Idara ya makosa ya jinai nchini Kenya (DCI) wanachunguza tukio la msichana mwenye umri wa miaka 15 anayedaiwa kuwaua wadogo zake watatu na binamu yake.
Taarifa za DCI zinasema msichana huyo anaesoma kidato cha kwanza katika kaunti ya Kiambu amekiri kutekeleza tukio hilo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Alikiri kwa wapelelezi kufanya maujai hayo na jinsi alivyowaua wadogo zake wenye umri wa miezi 15, miaka 5 na miaka 7 kati ya Februari na Julai 2021.
Mshukiwa pia alikiri mwezi uliopita alimuua binamu yake mwenye umri wa miaka 20 kwa kumzamisha kwenye kisima cha nyumba yao katika kijiji cha Kathiga kaunti ndogo ya Kabete.
DCI iliripoti
"Mtoto huyo alikir kutekeleza mauaji hayo mbele ya afisa wa watoto katika kaunti ndogo ya Kikuyu.Kwasasa anashikiliwa katika kaunti ya kikuyu huku wapelelezi wakimshughulikia ili aweze kufikishwa mahakamani."
0 Maoni