Rais wa Marekani Joe Biden anapanga kuzuru Florida baada ya kukumbwa na kile kinachohofiwa kuwa mojawapo ya vimbunga vilivyosababisha vifo vya watu wengi zaidi katika historia ya jimbo hilo.
Akizungumza katika makao makuu ya Shirika la Usimamizi wa Dharura (FEMA) ambalo limekuwa likiandaa misaada ya serikali kwa maafa ambayo yamesababisha uharibifu katika jimbo la kusini mwa peninsula, Biden amesema anahofia ‘hasara kubwa ya maisha’ kutokana na kimbunga Ian.
Takriban vifo sita vimeripotiwa, lakini idadi hii inatarajiwa kuongezeka huku waokoaji wakienea katika maeneo yaliyoathiriwa.
Gavana wa Florida Ron DeSantis amewaambia wanahabari kwamba jimbo hilo halijawahi kukabiliwa na dhoruba kubwa kama hiyo.
Kituo cha Kitaifa kinachoshughulikia masuala ya Vimbunga (NHC) kilitoa onyo katika ukanda wa pwani wa Carolina Kusini, wakati kimbunga Ian kikielekea kaskazini zaidi kwa upepo unaovuma kwa kasi ya mita 70 kwa saa.
Kwamsaada wa Mtandao
0 Maoni