TANGAZA HAPA

Kituo cha umeme Msamvu chapata hitilafu

                                    mtzonline255.tk

Meneja wa shirika la umeme nchini (TANESCO) kituo cha Morogoro mhandisi Fadhiri Chilombe amesema kituo cha kupokea,kupooza na kusambaza umeme cha Msamvu kimepata hitilafu na kusababisha maeneo mbalimbali kukosekana kwa huduma hiyo kwa masaa kadhaa.

Mhandisi Chilombe amesema hayo baada ya kutembelea kituo ambapo amesema kituo hicho kilipata hitilafu siku ya jana Septemba 14, 2022 ambapo mafundi wanaendelea na matengenezo.

Amesema kutokana na changamoto hiyo shirika linaendelea na mikakati ya kurejesha huduma katika hali ya kawaida kwa kuendelea na matengenezo.

Chilombe alisema maeneo yaliyoathirika zaidi baada ya kutokea kwa hitilafu katika kituo cha Msamvu ni maeneo ya Morogoro mjini,bwawa la mwalimu nyerere,mvomero na morogogo vijijini.

Aidhaa alisema hitilafu iliyotokea ni yakawaida katika maswala ya kiufundi na haihusiani na changamoto zilizokuwa zikitokea katika siku za nyuma kwenye kituo hicho.

Chapisha Maoni

0 Maoni