TANGAZA HAPA

MAKETE NJOMBE : Marufuku kula nyama ya nguruwe

 


Halmashauri ya wilaya ya Makete mkoni Njombe imepiga marufuku uchinjaji naulaji wa nyama ya nguruwe (Kitimoto) kwa muda usiojulikana kutokana na taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Afisa mifugo na uvuvi wa wilaya hiyo Aldo Mwapinga ametoa katazo hilo baada ya kutokea vifo vya nguruwe 21 wilayani humo alinukuliwa akisema,

"Kata ya Tandala kumeripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa ya nguruwe kwahiyo tutaenelea na jitihada za kuhakikisha tunashikiana na watendaji kuanzia ngazi ya kata hadi vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea".

Amesema serikali imepiga marufuku hiyo hususani katika kata ya Tandala huku akizuia utoaji wa nguruwe katika zizi moja kwenda jingine kwaajili ya upandisha kwa jike, vilevile akitaka kuacha kufukua nguruwe waliokufa (mizoga) na kuwachinja kisha kuenda kuuza nyama hizo vilabuni hii baada ya kupatikana kwa taarifa kuwa njia hiyo huwa inatumika.

Chapisha Maoni

0 Maoni