Kamati ya rufaa ya shirika la soka Tanzania TFF leo imetangaza maamuzi ya kamati hiyo kuhusiana na hukumu ya Haji Manara ya kufungiwa miaka miwili na kujihusisha na soka pamoja na faini ya shilingi milioni 20.
Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya maadili ya TFF Richard Mbaruku anasema wamepitia rufaa ya Haji Manara na kuona kuwa imekosa mashiko ila kwa kutumia busara ya kumpunguzia adhabu na sasa atatumikia kifungo chake cha miaka miwili kutojihusisha na soka na faini ya milioni 10 kutoka milioni 20 iliyokuwa awali.
July 21, 2022 Haji Manara alitangaziwa kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka na faini ya shilingi milioni 20 baada kukutwa hatia ya kumkosea nidha raisi wa TFF Wallace Karia wakati wa mchezo wa fainali za ASFC kati ya Yanga na Coastal Union katika uwanja wa Sheekh Amri Abeid jijini Arusha July 2, 2022.
0 Maoni