Mahakama ya hakimu mkazi Kiteto mkoani Manyara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela Yerenia Chidaka mkazi wa kijiji cha Dongo wilayani kiteto baada ya kufanya ngono na kumtia mimba mwanae wa miaka 16.
Mtuhumiwa amekiri kosa hilo mbele ya hakimu mkazi Mosi Sasy na kusema hataki kuisumbua mahakama na kusema aliamua kumpa mimba mtoto wake mtoto wake huyo ili asiolewe na mwanaume kabila la wakamba.
Imeelezwa kuwa baba huyo alipomweleza mkewe juu ya swala la kutotaka na mwanae aolewe na kabila la wakamba,mkewe alimjibu kwa dhihaka kwamba kama hataki mwanae aolewe basi amuoe yeye ndipo alipoamua kumpa ujauzito.
Alipotakiwa kujitetea mtuhumia aliomba mahakama impunguzie adhabu hiyo kwakua shetani alipitia kutenda kosa hilo huku mwendesha mashtaka wa polisi mahakamani hapo Inspekta Wilfred Mollel Alisema jeshi la polisi halina taarifa kama mtuhumiwa aliwahi kufanya kosa zaidi ya hilo na kuomba hakimu kumpa adhabu inayostahiki.
0 Maoni