Mkurugenzi wa ununuzi na ugavi wa mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) Ernest Khisombi amefikishwa mbele ya baraza ya maadili kwa tuhuma ya kujipatia mkopo wa gari binafsi yenye thamani ya shilingi milioni 196 kinyume na sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na.13 ya mwaka 1995.
Akisoma mashtaka mbele ya kamati ya maadili wakili wa serikali Hassan Mayunga aliambia baraza kuwa mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambazo ni kukopa fedha za mfuko ambazo ni kiasi cha TZS milioni 117.9 bila kufuata taratibu pamoja na kulipiwa kodi kiasi cha TZS milioni 78.8 bila kufuata utaratibu wasera za mikopo PSSSF.
Kwa mujibu wa Mayunga kitendo hichio kinamfanya Khisombi ambaye ni kiongozi wa umma kushindwa kufata matakwa ya kifungu cha 6(1) (a) na (b) na hivyo kukiuka maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu 6(2) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Hata hivyo Khisombi amekana tuhuma hizo na kulieleza baraza la maadili kuwa "fedha hizi ni haki yangu kama mkurugenzi wa ununuzi na ugavi kwa mujibu wa sera za mikopo ya mfuko".
0 Maoni