TANGAZA HAPA

Mume amkata mke mkono na titi

Maria Marwa Mkazi wa kijiji cha Isango wilayani Rorya mkoani Mara amekatwa mkono na titi na mume wake aliefahamika kwa jina la Werema Ibaso huku akijeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili hasa kichwani.

Tukio hilo lilitokea Septemba 7,2022 huku chanzo cha tukio hilo ikisemekana kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Maria alisema kuwa baada ya chakula cha usiku mumewe alimuomba simu yake na kutaka kujaza namba ambazo alikuwa nazo kwenye karatasi ili aone jina lililohifadhiwa katika simu.



Baada ya kugundua kuwa namba hiyo haijaifadhiwa katika simu ndipo alipoanzisha ugomvi akidai kuwa hiyo namba ni ya mwanaume mwingine alikuwa akiwasiliana nae kwa siri pasipo yeye kujua.

Imeelezwa kuwa baada ya ugomvi huo ndipo mwanaume huyo alipochukua panga na kuanza kumkata mama huyo kwenye mkono wake wa kushoto na titi lake la kushoto na kisha kumjeruhi maeneo mengine hasa kichwani kisha kukimbia kusikojulikana.

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime / Rorya Godfrey Sarakikya amekiri kutokea tukio hilo ambapo amesema jitihada za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea na mama huyo kwa sasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya mkoa ya rufaa mkoa wa Mara.

Chapisha Maoni

0 Maoni