Muuguzi wa Hospitali ya Amana Jijini Dar Es Salaam Joseph Mwampola (59) amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kusomewa mashtaka ya ubakaji na kulawiti.
Mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Yusto Ruboroga.
Inadaiwa mtuhumiwa hiyo alitenda makosa hayo katika maeneo mawili tofauti moja ikiwa ni ndani ya hospitali ya Amana ambapo inadaiwa alimbaka binti wa miaka 17 Februari mwaka huu.
Katika shitaka la pili inadaiwa mtuhumiwa alimbaka binti huyo katika nyumba ya kulala wageni mei 31 mwaka huu.
Mahakama imeeelza shtaka la tatu linalomkabili mtuhumiwa ni ulawiti ambapo inadaiwa Februari 22 Mwampola alimlawiti binti huyo katika hospitaliu ya Amana.
Kwa upande wa mshtakiwa alikana mashtaka hayo na mahakama kuahirisha kesi hadi Oktoba 5, 2022 na kwasasa mshtakiwa yupo nje kwa kutimiza masharti ya dhamana.
0 Maoni