Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amesema hana budi kulipa kisasi kwa mpinzani wake Liam Smith baada ya kupoza pambano kwa (TKO) jumamosi Septemba 3,2022.
Mwakinyo ametoa kauli hiyo na kusema kuwa hakuridhika na maamuzi dhidi yake kwenye pambano hilo.
"Sikufanyiwa haki katika pambano la juzi nimedhalilishwa vya kutosha dhidi ya mpinzani wangu nitahakikisha nalipa kisasi kwaajili yangu na ya watanzania" alisema mwakinyo
Pia kupitia ukurasa wake wa Instagram mwakinyo amethibisha kurudiwa kwa pambano hilo.
0 Maoni