TANGAZA HAPA

NJOMBE : Mbaroni kwa kumuua mtoto

                               

Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Happiness Mkolwe (27) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Jackson Kiungo (6) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ihanga na kujaribu kumfukia katika shimo alilokuwa amelichimba.

Kamanda wa polisi mkoani humo Hamisi Issah amethibitishwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikwenda kunyoa lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtuhumiwa alimfuata na kumchukua kisha kutoweka  nae kusikojulikana.

Amesema kuwa baada ya kufika huko mtuhumiwa alimsababishia kifo jackson na kumvua nguo kisha kumfukia kwenye shimo alilolichimba mwenyewe.

Kamanda anasema kisa kilichosababisha mauaji hayo kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ni kuwa wametengana na mume wake na kunamwanamke mwingine ambae ni mama wa mtoto huyo ambae alikuwa anakunywa pombe na mumewe hivyo alipopewa taarifa na watu wake aliamua kulipa kisasi.

Hata hivyo mtuhumiwa amekamatwa baada ya polisi kupata taarifa za kupotea kwa mwanafunzi Septemba 6, 2022. 

Chapisha Maoni

0 Maoni