Beki kutoka nchini Kenya Josh Onyango Achieng amefukunga juu ya sakata lake la kutaka kuvunjiwa mkataba wake Simba SC na kupelekea taharuki kubwa kwa mashabiki na wanachama wa msimbazi kwa kipindi cha mwezi uliopita.
Onyango amefunguka dhidi ya sakata hilo baada ya kumalizika kwa mchezo waliocheza na Tanzania Prisons uliochezwa jumatano septemba 14, 2022 uliomalizika kwa simba kushida 1-o ambapo alikiri kushinikizwa kuvunja mkataba wake.
Anasema sababu kubwa ya kufanya maamuzi kwenda kwenye kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF ni kutokana na mwenendo ambao hakuuona kuwa na mustakabali mzuri katika soka lake akiwa Simba SC.
Sababu nyingine iliyotajwa ni kuhusu mipango ya kocha Zorani Maki aliekuwa amekuja alisema kuwa siko katika mipango yake alisema Onyango
"Ni kweli niliomba kuondoka Simba kwasababu kocha alikuwa amekuja alisema kuwa sipo katika mipango yake,Ila kwa sasa mimi ni mchezaji wa Simba nitaendelea kuwepo na nitawaomba mashabiki waendee kutuombea na waje kwa wingi uwanjani"Alisema Onyango
0 Maoni