TANGAZA HAPA

Padri kizimbani kwa kesi ya kulawiti

 Sostenes Bahati Soka (41), Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita, Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro amesomeshwa mashtaka matatu katika Mahakama mbili tofauti,kwa kesi za madai ya kunajisi watoto watatu wenye umri chini ya miaka 12.

Katika kesi ya kwanza hakimu mkazi  mwandamizi mfawidhi Salome Mshasha,Wakili wa serikali Kassim Nasri,alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 12,2022 akiwa ofisi kwake.Wakili Nasri alidai mahakamani hapo kwamba mshtakiwa alitenda makosa hayo huku akijua ni kinyume na kifungu cha 130 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Wakili Nasri pia alidai kesi hiyo namba 45 ya mwaka 2022 mshatikiwa kwa makusudi alimbaka mtoto huo (Jina Limehifadhiwa) na baada ya kusomewa mashtaka hayo Padri Bahati alikana na hakimu Mshasha aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 10,2022.

Hata hivyo Padri Bahati alikosa dhamana baada ya kudaiwa barua za utambulisho za watu wawili waliopaswa kutia saini ya dhamana ya sh. milioni 10 kila mmoja.

katika kesi ya pili namba 44 ya mwaka 2022 katika mahakama ya hakimu mkazi moshi mbele ya hakimu mkazi Jennifer Edward mwendesha mashtaka wa serikali Kambarage Samson akisaidiana na Verdiana Mlenza alidaiwa mshtakiwa alimbana mtoto wa miaka 12.

Ilidaiwa mahakamani hapo mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti mwaka huu kinyume na kifungu cha 130 na 131 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshakiwa Padri Bahati alikana shtaka dhidi yake na hakimu Jennifer  alisema dhamana iko wazi kwa mujibu wa sheria.Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 18 kwaajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Katika shtaka la tatu lililosomwa katika Mahakama ya Wilaya Ya Moshi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Erasto Philly alidaiwa padri bahati alimbaka mtoto (jina limehifadhiwa) akisoma hati ya mashtaka mwandesha mashtaka Verediana Mlenza alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti mwaka huu hata hivyo mshtakiwa alikana shtaka dhidi yake na kesi kuahirishwa hadi Oktoba 12 mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE



Chapisha Maoni

0 Maoni