Jeshi la polisi limetoa ufafanuzi juu video fupi (Clip) iliyosambaa mtandaoni ikionyesha askari polisi akichukua fedha kwa raia wa kigeni baada ya mazungumzo ambayo yalionyesha ukiukwaji wa maadili ya jeshi la polisi.
Akitoa ufafanuzi huo leo hii Septemba 14, 2022 msemaji wa jeshi la polisi nchini kamishna mwandamizi wa polisi SACP David Misime alisema kuwa wanaosambaza video hiyo inaweza kuwa hawakupata mrejesho wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari huyo.
Anasema video hiyo ni ya tukio lililotokea katika mkoa wa Kaskazini Unguja miaka mitano iliyopita ambapo askari huyo alishtakiwa ndani ya siku tatu na kupatikan na hatia na alifukuzwa kazi huku polisi ikisema itaendelea kuwachukulia hatua kali askari wote watakaoenda kinyume na maadili ya jeshi la polisi.
0 Maoni