TANGAZA HAPA

Serikali yafuta tozo kuhamisha fedha Benki - Simu

Waziri wa fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba  amesimama Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho yatakayofanyika na kuanza kutumika kuanzia October 1, 2022.

Marekebisho aliyoyataja ni pamoja na Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya Benki moja (pande zote) na Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka Benki moja kwenda Benki nyingine (pande zote).

Mabadiliko mengine aliyoyataja ni pamoja na Wafanyabiashara (merchants) kutohusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni