Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) kanda ya ziwa magharibi imekama shehena ya sigara bandia aina ya SuperMatch zenye thamani ya Sh. 1.8 Bilioni.
Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 28, 2022 na meneja wa kitengo cha uhusiano TMDA Gaudensia Simwanza imeeleza kuwa walipokea taarifa kutoka mamlaka ya mapato Shinyanga.
"TMDA kanda ya ziwa magharibi baada ya kupokea taarifa ya kontena lenye bidhaa za tumbaku zilizozuiliwa katika ofisi ya TRA Shinyanga,imebaini sigara hizo ni bandia na zimeingizwa nchini kutoka nchi ya jirani ya Kongo ambapo kunamakasha 2200 yenye thamani ya Sh 1.8 Bilioni."
"Makasha hayo yanauzito wa tani 13.2 kazi hii kazi hii tulishirikiana karibu sana na MCIE lakini cha kujiuliza zimepitaje mipakani na tunao wakaguzi huko?Hatua zaidi zinaendelea kuchukuliwa na mzigo huu umezuiliwa" amesema Simwanza
CHANZO : MWANANCHI
0 Maoni