Klabu ya Simba SC imeweza kung'ara ugenini baada ya kuwachapa wenyeji Big Bullets bao 2-0 mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ligi ya mabingwa Afrika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa taifa Bingu nchini Malawi.
Moses Phiri aliweka bao la kwanza nyavuni dakika ya 29 na John Bocco aliandika bao la pili dakika ya 83.
Timu hizo zitarudiana tena Septemba 17 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam.
0 Maoni