TANGAZA HAPA

TABORA : Kibanda cha mlinzi kilichojengwa kwa milioni 11, Waziri mkuu atoa maagizo makali

 


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Tabora Musa Chaulo kuwakamata watu wote wanaohusika na usimamizi wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) wilayani Uyui kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo.

Amechukua hatua hiyo baada ya kukagua mradi huyo na kuonyesha kutoridhia na gharama ya baadhi ya majengo akiwemo kibanda cha mlinzi ambacho kimeweza kugharimu kiasi cha milioni 11 "Sitavumilia yeyote atakae mhujumu Raisi Samia Suluhu Hassan, watafutwe na wachukuliwe hatua" Alisema waziri mkuu

Waziri mkuu ametoa agizo hilo (Alhamisi Septemba 8, 2022) baada ya kukagua mradi huo wa chuo cha VETA ambapo amesema hajaridhishwa na ujenzi wa chuo hicho ambapo majengo yake yamejengwa kwa gharama kubwa tofauti na uhalisia  kwa kutumia mfumo wa nguvu kazi (force Account)

Mbali na ujenzi wa kibanda cha mlinzi pia waziri mkuu ameonyeshwa kutoridhishwa na ujenzi wa nyumba za watumishi chuoni hapo mabapo nyumba moja yenye uwezo wa kuchukua familia mbili gharama ni shilingi milioni 114 na tayari wameshatumia zaidi ya milioni 70 na bado haijaisha.

"Numba yenye uwezo wa kuchukua familia tatu wizara ya Afya inajenga kwa shilingi milioni 90 ofisi ya Rais (TAMISEMI) wanajenga nyumba za walimu zenye uwezo wakuchukua familia mbili wa gharama ya shilingi milioni 57 na wanajenga kwa mfumo wa force account kama wanavyojenga hapa hii haikubaliki" Alisema waziri mkuu

Kutokana na kutorishwa na ujenzi wa chuo hicho unaosimamiwa na VETA mheshimiwa majaliwa amemuagiza mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani asimamie ujenzi wa chuo hicho ili uweze kukamilika kwa wakati "mkuu wa mkoa simamia ujenzi wa chuo hichi na ukamilike kwa wakati" Alisema waziri mkuu.

Chapisha Maoni

0 Maoni