TANGAZA HAPA

tetesi za soka Ulaya 22.09.2022

Borussia Dortmund inamthamini kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, anayelengwa na Manchester United na Liverpool, kwa takriban £130m. (Athletic - subscription required)

Kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 25, anasema "siku zote alitaka kusalia Barcelona" baada ya kukataa uhamisho wa £65m kwenda Manchester United wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Juventus Manuel Locatelli, 24, amehusishwa na uhamisho wa Arsenal. Muitaliano huyo ameshindwa kumfurahisha bosi Massimiliano Allegri tangu alipohamia timu hiyo kwa pauni milioni 30 kutoka Sassuolo. (Calciomercato via Sun)



Arsenal wamewasiliana na kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt Jesper Lindstrom, 22, kuhusu uhamisho wa pauni milioni 17 kwa raia huyo wa Denmark mwezi Januari. (Bild - in German)

Makamu wa rais wa Flamengo anasema "hakuna ombi" kwa Joao Gomes, 21, huku kiungo huyo wa kati wa Brazil akihusishwa na Liverpool na Manchester United (ESPN - in Portuguese)

Manchester United iliripotiwa kuwa na nia ya kumpeana kiungo wa Ubelgiji Andreas Pereira, 28, kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na Gomes msimu wa joto, kabla ya Pereira kujiunga na Fulham. (Talksport)


Hakuna klabu iliyofikia bei iliyotakiwa msimu wa joto kwa winga wa PSV Eindhoven wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, ambaye alihusishwa na kuhamia Manchester United, Southampton, Leeds United na Arsenal. (Voetbal International via TalkSport)

Kiungo wa kati wa Newcastle United Elliot Anderson, kinda kutoka shule ya mafunzo ya soka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 19, ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu katika klabu hiyo. (Chronicle)

Meneja wa Celtic Ange Postecoglou anasema kuondoka kuchukua mikoba ya Leicester City "haiko kwenye rada yangu". (Sky Sports)


Kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Sergio Busquets, 34, yuko tayari kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Inter Miami, inayomilikiwa na David Beckham, mwishoni mwa kandarasi yake msimu ujao wa joto. (Sport - in Spanish)

Nyongeza ya kandarasi ya miaka miwili iliyotiwa saini mwezi Julai na kiungo wa kati wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 25, ilijumuisha kipengele cha €50m (£43.7m), ambacho kitakuwa halali kuanzia msimu ujao wa joto. Dembele angepokea nusu ya ada hiyo baada ya kukubali kuondoa bonasi yake. (L'Equipe - in French)

Meneja wa Rotherham United Paul Warne anapendekezwa kuchukua kibarua cha kuifunza Derby County baada ya Rams kumfuta kazi kocha wa muda Liam Rosenior. (Yorkshire Post)


SOURCE ; BBCSWAHILI

Chapisha Maoni

0 Maoni