TANGAZA HAPA

Tetesi za soka Ulaya 23.09.2022


Usajili wa Paris St-Germain wa nyota wa Argentina Lionel Messi, 35, kutoka Barcelona kwa uhamisho wa bila malipo mnamo Agosti 2021 hadi sasa umeiingizia klabu hiyo ya Ligue 1 mapato ya euro 700m (£612m) kutokana na mikataba ya kibiashara. (El Economista via Mirror)  

Leicester City wananuia kumpa meneja aliye chini ya presha Brendan Rodgers muda zaidi wa kubadilisha mambo katika klabu hiyo iliyo mkiani mwa Ligi Kuu ya Uingereza. Hata hivyo, mapokezi anayopata kutoka kwa mashabiki kwenye mechi ya nyumbani dhidi ya Nottingham Forest yanaweza kuwa muhimu kwa mustakabali wa raia huyo wa Ireland Kaskazini katika klabu hiyo. (The Athletic - subscription required)  

Mazungumzo ya kandarasi kati ya Everton na Anthony Gordon "yanaendelea vyema" huku mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, aliyehusishwa na uhamisho wa  Chelsea msimu wa joto, akitazamia nyongeza "kubwa" ya malipo. (inews - subscription required)  

Kocha wa zamani wa Bournemouth na kiungo wa kati wa England Scott Parker, 41, ameibuka kuwa mtu anayetarajiwa kuchukua mikoba ya ukufunzi katika klabu ya Nice.. (Foot Mercato via Sun)  

Kipa wa Denmark Kasper Schmeichel, 35, amekuwa na matokeo mabaya kwa mara ya kwanza katika klabu ya Nice tangu uhamisho wake kutoka Leicester City, baada ya kuwasili akiwa mzito na kuwasumbua wasimamizi na wachezaji wenzake kwa kukiuka sheria za klabu. (RMC Sport via Sun) 

 Beki wa Korea Kusini Kim Min-jae, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United, ana kipengele cha kutolewa katika mkataba wake wa Napoli wa takriban euro 50m. Lakini, kwa vile haiwezi kuanzishwa katika dirisha la uhamisho la Januari, klabu yoyote inayotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 italazimika kusubiri hadi msimu ujao wa joto. (Gianluca Di Marzio)  

Barcelona watakuwa na chaguo la kusitisha mkataba wa beki wa kati wa Uhispania Gerard Pique mnamo Juni 2023 - mwaka mmoja mapema - iwapo beki huyo mwenye umri wa miaka 35 atashiriki katika chini ya 35% ya mechi zote msimu huu. (Mundo Deportivo)

 Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 28, anasema "miaka michache iliyopita katika Juventus haikuwa rahisi" na mabadiliko ya kuhamia Roma msimu wa joto "yalinisaidia". (ESPN Argentina, via Football Italia)

 Meneja wa zamani wa Barcelona Ronald Koeman anasema alitaka kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 31, alipokuwa akiinoa klabu hiyo ya Uhispania lakini alishindwa kwa sababu rais wa klabu Joan Laporta "alitaka kuniudhi zaidi kuliko kuleta mchezaji". (AD, via Goal)

Mmiliki wa AC Milan Gerry Cardinale atarejea Italia mnamo Oktoba wakati nyingeza ya kandarasi kwa meneja Stefano Pioli na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao, 23, kutakuwa miongoni mwa vipaumbele vyake. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)

 Kiungo wa kati wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 21, anavutia macho kama nambari 10 baada ya kuanza mechi nne mfululizo akiwa kwa mkopo kutoka Chelsea katika klabu ya Bayer Leverkusen. (The Athletic - subscription required) 

Mchezaji wa Argentina Mauricio Pochettino, 50, atasubiri kazi ya kiwango cha juu nchini Uingereza, Uhispania au Italia na hataki kuchukua nafasi ya kuwa mkufunzi mkuu katika klabu ya Nice ya Ufaransa. (Evening Standard)

Source : BBCSWAHILI

Chapisha Maoni

0 Maoni