TANGAZA HAPA

Tetesi za soka Ulaya 24.09.2022

Juventus wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Wolves wa Uhispania Adama Traore, 26, wakati dirisha la uhamisho la Januari litakapofunguliwa. (Birmingham Mail)

Juventus pia wanamtaka mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 31, ambaye yuko kwa mkopo Atletico Madrid kutoka Barcelona, ​​pamoja na kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 26, na winga wa Chelsea wa Marekani Christian Pulisic, 24. (Football Italia )

Barcelona wanawania kukamilisha dili la pauni milioni 22 kwa ajili ya uhamisho wa kudumu wa Griezmann kwenda Atletico Madrid. (Mail)


Arsenal wanaweza kuwekewa dau la £101m mara mbili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic wa Serbia mwenye umri wa miaka 22 na kiungo wa kati wa Italia Fabio Miretti, 19. (Sun)

The Gunners pia wamewasiliana na Eintracht Frankfurt kuhusu winga wa Denmark mwenye umri wa miaka 22 Jesper Lindstrom. (Mail) 

Beki wa Uingereza Trevoh Chalobah, 23, amehusishwa na tetesi za kutaka kuondoka Chelsea huku Roma ya Jose Mourinho ikitarajiwa kumununua mwezi Januari. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)


Klabu ya Nice ya Ufaransa imekana kumlenga kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kama meneja wao mpya, na inasemekana kumtaka kocha wa zamani wa Bournemouth Scott Parker. (Sun)

Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool na Manchester City zinamfuatilia kiungo wa kati wa Uhispania na Villarreal mwenye umri wa miaka 21 Alex Baena, ambaye ana kipengele cha kuweza kuondoka cha euro milioni 35. (Sport - kwa Kihispania)

Chelsea na Manchester City pia wanavutiwa na mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, ambaye thamani ya inadaiwa kuwa zaidi ya £100m. (Habari za jioni za Manchester)


Mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte yuko tayari kurejea Juventus msimu huu iwapo Massimiliano Allegri atatimuliwa kwa sababu ya kiwango chake duni. (Star)

Eden Hazard amezungumza kuhusu hali yake "tete" katika klabu ya Real Madrid na mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 31 anatamani kupata muda zaidi wa kucheza kabla ya Kombe la Dunia. (ESPN).


SOURCE ; BBCSWAHILI

Chapisha Maoni

0 Maoni